(naibu wazi wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto akijibu swali bungeni)
Serikali kupitia wizara ya afya,maendeleo ya
jamii,jinsia wazee na watoto
imesema bado inasikitika kuona ukiukwaji wa huduma za afya,haki za fya
na haki za uzazi katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Akijibu swali bungeni naibu waziri wa afya,maendeleo
ya jamii,jinsia wazee na watoto Dakta HAMIS KIGWANGALA amesema tafiti
zinaonyesha kuwa suala hilo linadumaza matumizi ya huduma na kuhatarisha maisha
ya wanawake.
Dakta KIGWANGALA amesema serikali ina jukumu la
kutoa na kusimamia utoaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto na jukumu hilo
linatekelezwa kwa tumia vituo vya kutolea huduma za afya ya uzazi na mtoto vya
umma na binafsi kote nchini.
Aidha naibu waziri ameeleza kuwa huduma hizo
hutolewa kwa kuzingatia haki za wateja kama ilivyoainishwa kwenye miongozo ya utoaji wa huduma hizo.
Hata hivyo dakta KIGWANGALA amesema katika
kuhakikisha haki hizo zinapatikan serikali kwa kupitia mifumo yake ikiwa mabaraza ya weledi zitatoa
mafunzo kwa watoa huduma za afya kuhusiana na haki za wateja na mahitaji muhimu
ya mtoa huduma na haki ya kutumia huduma kwa hiari pasipo shuruti.
Lakini pia ameeleza kuwa katika kutekeleza hilo vituo vya kutolea huduma za afya vinavisanduku vya maoni na ofisi za malalamiko ambazo ni sehemu muhimu ambapo wateja wanaweza kupelekeka malalamiko yao ili hatua zaidi zichukuliwe kukomesha na kutokomeza ukiukwaji wowote wa haki za binadamu.
Binde/bunge