Alhamisi, 13 Agosti 2015







 MBIO ZA URAIS TANZANIA NA POMBE MAGUFULI.
Ni katika hali ya furaha na shangwe juu ya uteuzi wa mweshimiwa POMBE JOHN MAGUFULI kusimanishwa na rais JAKAYA MRISHO KIKWETE katika kugombea nafasi ya urais....2015


 


Hatimaye kile kilicho kuwa kinasubiriwa kwa muda mrefu katika mkutano mkuu wa  chama cha mapinduzi -CCM- mkoani DODOMA kimejidhihirisha .

Zilianza mbio na heka heka za makada wa chama cha mapinduzi kuchukua fomu na kila mmoja kutangaza kwa nafasi yake kuwania kugombea kiti cha uraisi ambapo katika makada hao waliokuchukua fomu walifikia arobaini na mbili (42).

Zoezi hilo liliendelea na hatimaye ikafika wakati wa kila mmoja kurudisha fomu za uraisi ambapo pia katika kurudisha fomu hizo makada thelatini na nane walirudisha fomu na wanne hawakurudisha fomu hizo.

katika mkutano huo wa CCM ulianza mchakato wa mchujo ili kupata tano bora ambapo katika mchujo huo walipatikana waanawake wawili na wanaume watatu.

Hata hivyo huko kote ni katika kinyang'anyiro ya kutaka kiti cha uraisi au kutia guu IKULU,watano hao waliye chaguliwa ni pamoja na aliye kuwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa (UN) Dakta ASHA ROSE MIGIRO,Balozi AMINA SALUMU ALI, Waziri wa ujenzi Dakta JOHN POMBE MAGUFULI, naibu waziri wa sayansi na teknolojia  mh.JANUARY YUSUF MAKAMBA,na waziri wa mambo ya nje BERNAD KAMILIUS MEMBE.

Mchakato wa kuendelea kutafuta nani atakae ipeperusha bendera ya CCM hatimaye taifa ukaendelea na kuwatafuta watatu ambao walipatikana,watau hao ni pamoja na Dakta,ASHAROZI MIGIRO,Balozi AMINA SALUMU ALLY na Dakta JOHN POMBE MAGUFULI.

Hatimaye ukafika wakati wa kumtafuta mmoja kati ya wale watatu kwa kupiga kura na wajumbe mbali mbali walioshiriki katika mkutano huo wa CCM ambapo alipatikana mmoja huyo naye ni Dakta JOHN POMBE MAGUFULI ndiye atakae peperusha bendera ya chama hicho katika kampeni za uraisi licha ya kuwepo kwa vyama mbalimbali vya upinzani.

Hata hivyo, kupatikana  kwa mgombea huyo kuwania kiti cha urais kutaleta chachu na tija kwa wananchi kuondokana na umasikini ambao umekua ni kiilio miaka mingi kwa wananchi wa TANAZNIA .





Alhamisi, 26 Februari 2015

MAONI
  DODOMA

Wananchi mkoani DODOMA wameiomba serikali  kuandaa vifaa ,mapema kwenye vituo vya kujiandikishia  kwa wakati ili kuepusha usumbufu ambao utajitokeza kwa wananchi katiaka zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura .
   Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa mkoa wa DODOMA  wameeleza kuwa serikali inatakiwa kuaangalia mapema mapungufu mbalimbali ili katika mfumo unaotumika kwa sasa.
    Hata hivyo wameitaka serikali kuendelea kutoa elimu zaidi  ya matumizi ya mfumo unaotumika sasa katika zoezi la kijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kutokupoteza haki yao ya msingi ya kupiga kura.
     Mbali na hayo  akizindua  daftari la uboreshaji la wapiga kura mkoani NJOMBE wilaya ya MAKAMBAKO waziri mkuu wa TANZANIA  MIZENGO PINDA amewataka viongozi wa siasa kuwahamasisha wananchi kwa wingi kujitokeza katika zoezi la kijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura bila kujali itikadi za kisiasa.    



Ijumaa, 20 Februari 2015



MIKOPO

DODOMA

Wajasiriamalimkoani DODOMA wameiomba Serikali kushirikiana na taasisi mbalimbali za mikopo zitakazowasaidia kuwakopesha fedha kwa masharti nafuu  ili waweze kukopa na kujikwamua kimaisha.

Wakizungumza na TBC, baadhi ya wajasiriamali wanaojishughulisha na shughuli za useremala katika eneo la MAJENGO mjini DODOMA wamesema kuwa, taasisi nyingi za kibenki zimekuwa zikiangalia mali walizonazo wajasiriamali kabla ya kuwakopesha hatua inayowakwamisha kukopa katika benki hizo.

 Aidha  wajasiriamali hao wamesema  juhudi kubwa wanazozifanya ni pamoja na kuboresha bidhaa wanazozitoa katika uzalishaji ili ziwe bora kwa lengo la kuwavutia wateja.

 Tatizo jingine linalowakabili wajasiriamali hao ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kuzalishia bidhaa, upatikanaji wa  mitaji na mzunguko wa biashara kuwa mgumu.

Wametoa wito kwa vijana kujishughulisha kufanya kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kupiga soga huku wakitegemea kuajiriwa serikalini.


KERO YA MAJI

CHEMBA

Wananchi wakijiji cha kata ya makorongo wilayani chemba mkoani Dodoma wameiomba serikali kuwasaidia kuondokana na kero ya maji ambayo imekua ikiwasumbua kwa muda mrefu na kuwalazimu wananchi hao kufuata huduma ya maji kwa umbali mrefu.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho FATUMA KITAMBI amesema kuwa kero hiyo kwa sasa imekua sugu kutokana na ubovu wa mashine wanayoitumia katika uzalishaji maji,na wakati mwingine huwalazimu kukopa fedha kwa wadau na kuendesha shughuli za uzalishaji maji
 
Naye mganga mfawidhi wa kituo cha afya  cha makorongo bahati mohamedi amesema kuwa athari wanazoweza kupata wananchi kutokana na kutumia maji yasiyo safi na salama ni pamoja na kupata magonjwa ya mlipuko kama vile kuharisha damu na ukosefu pamoja na ukosefu wa maji.
www.halfanbinde.blogsport.com 
Hata hivyo wananchi hao wamesema kwamba changamoto ambazo hukumbana nazo ni pamoja na kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za uzlishaji.