KERO YA MAJI
CHEMBA
Wananchi wakijiji cha kata ya makorongo wilayani chemba mkoani Dodoma wameiomba serikali
kuwasaidia kuondokana na kero ya maji ambayo imekua ikiwasumbua kwa muda mrefu na
kuwalazimu wananchi hao kufuata huduma ya maji kwa umbali mrefu.
Mwenyekiti
wa serikali ya kijiji hicho FATUMA KITAMBI amesema kuwa kero hiyo kwa sasa
imekua sugu kutokana na ubovu wa mashine wanayoitumia katika uzalishaji maji,na
wakati mwingine huwalazimu kukopa fedha kwa wadau na kuendesha shughuli za
uzalishaji maji
Naye mganga
mfawidhi wa kituo cha afya cha makorongo
bahati mohamedi amesema kuwa athari wanazoweza kupata wananchi kutokana na
kutumia maji yasiyo safi na salama ni pamoja na kupata magonjwa ya mlipuko kama
vile kuharisha damu na ukosefu pamoja na ukosefu wa maji.
www.halfanbinde.blogsport.com
Hata hivyo
wananchi hao wamesema kwamba changamoto ambazo hukumbana nazo ni pamoja na
kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za uzlishaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni