MIKOPO
DODOMA
Wajasiriamalimkoani DODOMA wameiomba Serikali kushirikiana na taasisi mbalimbali za mikopo zitakazowasaidia
kuwakopesha fedha kwa masharti nafuu ili
waweze kukopa na kujikwamua kimaisha.
Wakizungumza
na TBC, baadhi ya wajasiriamali wanaojishughulisha na shughuli za useremala
katika eneo la MAJENGO mjini DODOMA wamesema kuwa, taasisi nyingi za kibenki
zimekuwa zikiangalia mali walizonazo wajasiriamali kabla ya kuwakopesha hatua
inayowakwamisha kukopa katika benki hizo.
Aidha wajasiriamali
hao wamesema juhudi kubwa wanazozifanya
ni pamoja na kuboresha bidhaa wanazozitoa katika uzalishaji ili ziwe bora kwa
lengo la kuwavutia wateja.
Tatizo jingine linalowakabili wajasiriamali
hao ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kuzalishia bidhaa, upatikanaji wa mitaji na mzunguko wa biashara kuwa mgumu.
Wametoa wito
kwa vijana kujishughulisha kufanya kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na
kupiga soga huku wakitegemea kuajiriwa serikalini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni