DODOMA
Wananchi mkoani DODOMA wameiomba serikali kuandaa vifaa ,mapema kwenye vituo vya
kujiandikishia kwa wakati ili kuepusha
usumbufu ambao utajitokeza kwa wananchi katiaka zoezi la uandikishaji katika
daftari la kudumu la wapiga kura .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa mkoa wa
DODOMA wameeleza kuwa serikali inatakiwa
kuaangalia mapema mapungufu mbalimbali ili katika mfumo unaotumika kwa sasa.
Hata hivyo wameitaka serikali kuendelea kutoa elimu
zaidi ya matumizi ya mfumo unaotumika
sasa katika zoezi la kijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili
kutokupoteza haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Mbali na hayo
akizindua daftari la uboreshaji
la wapiga kura mkoani NJOMBE wilaya ya MAKAMBAKO waziri mkuu wa TANZANIA MIZENGO PINDA amewataka viongozi wa siasa
kuwahamasisha wananchi kwa wingi kujitokeza katika zoezi la kijiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura bila kujali itikadi za kisiasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni